Serikali ya Victorian inatoa msaada kwa shule zote shule za chekechea zikijumuishwa katika maeneo ambayo yame athiriwa na mafuriko. Familia zitaweza watuma watoto wao wenye kati ya miaka 3 hadi 4 kupokea huduma yamalezi ya watoto bure katika mhula wa tatu. Wanafunzi wanao jiandaa kufanya mitihani ya V-C-E, wataweza tumia matokeo ya mtihani maalum katika mitihani yao.
Vyombo vya habari vya Uganda pamoja na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu Jumatatu wamewasilisha shauri mahakamani kupinga sheria mpya yenye utata kuhusu matumizi ya intaneti, ambayo wanasema inalenga kuzuia uhuru wa kujieleza na kuwanyamanzisha wapinzani. Kulingana na ombi hilo, serikali imepewa siku saba kuwasilisha utetezi wake lakini haijulikani lini kesi hiyo itaanza kusikilizwa.
Rais wa Kenya Dr Ruto, amevunja kikosi cha 'polisi wauaji'. Hatua hiyo inajiri baada ya kiongozi huyo kupokea ripoti ya uchunguzi kuhusu kutoweka kwa raia wawili wa India na mwenyeji wao aliyekuwa dereva wa gari walimokuwa. Ripoti hiyo ilipendekeza kuvunjiliwa mbali kwa kitengo hicho ili kuruhusu uchunguzi kukamilika kabla ya faili hiyo kuwasilishwa kwa mkurugenzi mkuu wa mashtaka nchini kenya.