Taarifa ya Habari 18 Septemba 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Kaimu waziri mkuu Richard Marles atetea jibu rasmi la serikali ya Australia, kwa kifo cha Malkia Elizabeth wa pili.


Walimu wanaongoza kampeni kwa serikali ya shirikisho kuhakikisha kuwa takriban idadi yawanafunzi 40, wanao jiandaa kufanya mitihani yao ya darasa la 12, wapewe makazi yakudumu ili waweze fanya elimu yao ya juu. Wanafunzi hao ni sehemu ya kundi la watu elfu 19 ambao, wamekuwa waki ishi nchini kwa visa ya mpito, chini ya sera inayo waathiri waomba hifadhi walio wasili nchini kwa boti.

Mji wa Brisbane unajiandaa kuwa mwenyeji wa kwanza wa kongamano la kanda, kwa namna yakupunguza hatari za janga tangu mwanzo wa wa Coronavirus. Takriban wajumbe 4,000 kutoka nchi 38 wamewasili mjini humo kwa kongamano la siku nne [[19-22 Sept]] kwa jina la Asia-Pacific Ministerial Conference on Disaster Risk Reduction.

Maafisa nchini Eritrea wametoa wito kwa vikosi vyao vya kijeshi kukusanyika ili kukabiliana na mapigano mapya kaskazini mwa Ethiopia. Tahadhari ya kusafiri iliyochapishwa mwishoni mwa juma na serikali ya Canada na Uingereza iliwaonya raia wao walio nchini Eritrea kupunguza safari zao kufuatia wito huo. Kurejea kwa mapigano mwezi uliopita yalouvunja mpango wa kusitisha mapigano uliofikiwa mwezi Machi kati ya serikali ya Ethiopia na waasi wa Tigray.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service