Migogoro ndani ya chama cha Liberal juu ya chaguzi la Scott Morrison kwa mgombea wa eneo bunge la Warringah unaendelea, mweka hazina wa New South Wales akisema mgombea huyo anapashwa vuliwa ugombea wake. Hata hivyo waziri mkuu amekana wito wakumvua ugombea Bi Deves, akisema anamengi yakutoa kwa jamii.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Jumatatu ametangaza kuwa mafuriko mabaya yanayolikumba taifa hilo ni janga la kitaifa, na kuonya kwamba ukarabati wa huduma za msingi utachukua muda mrefu. Rais Ramaphosa amesema hayo katika hotuba kupitia televisheni ya taifa “Hili ni janga la kibinadamu ambalo linahitaji juhudi kubwa na za haraka za kutoa msaada. Maisha, afya na ustawi wa maelfu ya watu bado vipo hatarini” aliongeza.
Watu kadhaa wamejeruhiwa katika shambulizi la mizinga dhidi ya bunge la Somalia wakati wabunge walikuwa wakikutana kwa mara ya pili tangu walipoapishwa wiki iliyopita. Hakuna mbunge amejerihiwa katika shambulizi hilo dhidi ya jengo lenye ulizi mkali sana mjini Mogadishu, na ambalo kundi la kigaidi la Al-shabaab limedai kutekeleza. Bunge la Somalia lipo karibu na ikulu ya rais, katikati mwa mji mkuu wa Mogadishu.