Taarifa ya Habari 19 Disemba 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Mvua kubwa na kali ambayo imegonga eneo la Kaskazini Queensland ina anza kupungua ukali ila, ofisi ya utabiri wa hewa imesema onyo za mafuriko bado zina endelea kutumika.


Vituo vya uhamisho vime andaliwa kwa watu katika eneo la kaskazini magharibi New South Wales, ambako wakaaji wanakimbia moto katika eneo la Duck Creek ambalo liko katika msitu wa Pilliga, kusini ya Narrabri. Moto huo ume haribu zaidi ya hekta elfu 85 na ume orodheshwa kuwa haudhibitiki.

Shirika la Scamwatch limesema wa Australia wamepoteza zaidi ya dola milioni 7, kwa ulaghai wa kuemea mtandaoni mwaka mzima kufikia Novemba. Sasa, wiki moja kabla ya krismasi, makampuni makubwa ya simu pamoja na mchunguzi wa kitaifa wa wateja, amewaonya watu wafanye tahadhari zaidi wanapo nunua zawadi mtandaoni. Kampuni ya Telstra imesema imeona ongezeko la 66% kwa ulaghai wa jumbe za maandishi fupi kulinganisha na mwaka jana.

Waziri wa shirikisho wa uhamiaji Andrew Giles anakutana na washirika wake wamajimbo na wilaya mjini Canberra hii leo, kwa mazungumzo kuhusu uhamiaji. Uteuzi wa viza kwa kila mamlaka utajadiliwa, wakati mawaziri wana zingatia mbinu zaku shughulikia uhaba wa ujuzi. Serikali ya shirikisho inataka rejesha idadi za uhamiaji wa kila mwaka kwa viwango vya kabla ya janga.

Kenya na Umoja wa Ulaya zimetia saini makubaliano ya kibiashara yaliyojadiliwa kwa muda mrefu ili kuongeza mtiririko wa bidhaa kati ya masoko hayo mawili. Hayo yamefahamishwa na Rais William Ruto katika wakati ambapo Brussels ikilenga kukuza mahusiano ya kiuchumi na bara la Afrika.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amesema uchaguzi mkuu wa siku ya Jumatano utafanyika katika mazingira ya kuaminika. Lakini mivutano imeongezeka kutokana na ukosefu mkubwa wa maandalizi jambo linaloweza kusababisha migogoro katika taifa hilo.

Kampuni ya kutengeneza chanjo za Covid-19 ya BioNtech inalenga kuanza utengenezaji kwenye kiwanda chake cha chanjo cha mRNA chini Rwanda kufikia 2025, maafisa wake wamesema Jumatatu, ikiwa kampuni ya kwanza ya kigeni kutengeneza chanjo hizo barani Afrika.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 19 Disemba 2023 | SBS Swahili