Mamlaka ya udhibiti wa madawa ya Australia imetoa idhini ya muda kwa chanjo ya dawa ya Moderna ya UVIKO-19 kwa watoto wachannga. Utawala wa bidhaa za tiba imetoa idhini ya muda kwa dozi za watoto wenye kati ya miezi sita hadi miaka tano, uamuzi wake ukishawishiwa na data kutoka idadi ya watoto elfu sita walio pokea chanjo ya moderna iliyo fanyiwa mageuzi katika majaribio katika nchi za Canada na Marekani.
Serikali ya Tanzania imebaini kuwa ugonjwa unaoua watu kusini mwa Tanzania ni homa ya Mgunda. Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu amewaambia waandishi wa habari kuwa upimaji wa sampuli za wagonjwa waliokuwa wakiugua katika Wilaya ya Ruangwa katika Mkoa wa Lindi umethibitisha mlipuko huu kuwa wa ugonjwa unaoitwa kitalaamu Leptospirosis, Field Fever au kwa lugha ya Kiswahili inajulikana kama Homa ya Mgunda.
Australia yajirusha dimbani kuwa mwenyeji wa kombe la Asia mwakani, baada ya China kujiondoa, na mataifa ya Afrika yaendelea kujiuliza maswali baada ya matokeo mabaya katika michuano ya riadha mjini Oregon Marekani.