Vikundi vinavyo wakilisha viwanda vimesema mpango wa serikali ya Victoria, wakuondoka katika makatazo una maana biashara nyingi hazitaweza kufunguliwa tena hadi mwanzo wa Novemba. Mabaa, vilabu na kumbi za burudani mjini Melbourne zinaweza wapokea wateja 50 ambao wamepokea chanjo kamili katika sehemu za nje na, vinyozi pamoja na wanao toa huduma binafsi wanaweza fungua biashara zao tena kuwa hudumia wateja watano ambao wamepokea chanjo kamili wakati ambapo 70% yawatu wa Victoria watakapo kuwa wamepokea chanjo kamili.
Kiongozi wa NSW Gladys Berejiklian ametangaza kuwa vizuizi vitaregezwa katika halmashauri za jiji 12 za wasiwasi kuanzia kesho Jumatatu septemba 20, hatua ambayo itaweka maeneo hayo kuwa sawa na sehemu zingine za Sydney. Tangazo hilo limejiri wakati jimbo la NSW limerekodi kesi mpya 1,083 za maambukizi ya COVID-19 ndani ya jamii, pamoja na vifo 13 vya ziada.
Viongozi wa majimbo huko Somalia Ijumaa walitoa wito kwa Rais na Waziri Mkuu kumaliza ugomvi wao wakionya juu ya hatari ya kutokuwa na utulivu wa kisiasa katika taifa hilo la Pembe ya Afrika. Mzozo huo uliongezeka kwa haraka Alhamisi, wakati Rais Mohamed Abdullahi Mohamed, ambaye ni maarufu kama Farmajo, aliposimamisha mamlaka ya utendaji ya Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble. Kitendo hicho kilipingwa mara moja na Waziri Mkuu na kueleza kwamba kinakwenda kinyume na sheria.