Mfanyakazi katika meli iliyo tia nanga kusini mwa Perth, amepatwa na COVID-19. Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 20, ina aminiwa ni mpishi katika meli hiyo na, alisafirishwa katika karantini ya hoteli kwa gari la dharura jana usiku kutoka kituo cha Kwinana Bulk Terminal. Kiongozi wa jimbo hilo Mark McGowan amesema zaidi ya idadi ya wafanyakazi 20 ndani ya meli hiyo, kwa jina la Allegra, hawaja onesha dalili zozote za virusi hivyo.
Watu angalau 55 waliuawa katika mashambulizi mawili ya usiku kucha kwenye vijiji huko mashariki mwa Congo, Umoja wa Mataifa ulisema Jumatatu katika usiku ambao ulikuwa mbaya sana kwenye eneo ambalo limeshuhudia ghasia katika kipindi cha takriban miaka minne.
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amesema nchi yake iko tayari kuimarisha ushirikiano wake na Kenya pamoja na jamii ya kimataifa. Na Tanzania na Kenya zimetia saini makubaliano ya kuondoa vikwazo vya kibiashara ambavyo vilikuwa vikizuia ushirikiano mzuri wa kufanya biashara.