Taarifa ya Habari 2 Aprili 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Kiongozi wa Victoria amesema kushindwa kwa chama cha Liberal katika chaguzi dogo la Aston, kume onesha wapiga kura wanaendelea kutupilia mbali aina chafu ya siasa.


Kiongozi mpya wa New South Wales Chris Minns amesema haamini hali ya serikali ya wachache ya chama cha Labor itakuwa kizuizi. Maandamano kadhaa yamefanyika kote nchini Australia mapema hii leo, kuwaunga mkono wakimbizi ambao bado wanaishi katika hali ya sintofahamu ndani ya vizuizi vya uhamiaji.

Wanasheria wanaomuwakilisha rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, wameapa kwamba mteja wao hatosaka tena makubaliano nje ya mahakama na badala yake yuko tayari kupambana dhidi ya mashitaka yote dhidi yake.

Mapigano mapya yamezuka Jumamosi asubuhi katika mji unaogombaniwa wa Las’anod nchini Somalia, si chini ya miezi miwili baada ya serikali ya Marekani kutaka kuondolewa kwa wanajeshi katika eneo hilo. Viongozi wa Sudan wameahirisha kutiwa saini kwa makubaliano yaliyopangwa kufanyika Jumamosi ili kurejesha kipindi kifupi cha mpito cha kidemokrasia, afisa mmoja amesema, huku hali ya kutoelewana ikiendelea kati ya makundi ya kijeshi.

Ombi la msamaha la bingwa wa zamani wa michezo ya Olimpiki kwa walemavu raia wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, aliyefungwa jela mwaka 2016 kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp limekataliwa. Haya ni kulingana na mamlaka za magereza Afrika Kusini na wakili wa familia ya Steenkamp.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 2 Aprili 2023 | SBS Swahili