Kwa mara ya kwanza watu wenye viza ya muda wanao kimbia unyanyasaji wa nyumbani, watapata kiwango sawia cha msaada kutoka serikali ya shirikisho sawia na raia wa Australia. Mwanamke mmoja kati ya wanawake sita nchini, hupitia unyanyasaji wa nyumbani, wakati katika wahamiaji na wakimbizi ni mwanamke mmoja kati ya wanawake watatu.
Kikosi cha Umoja wa Afrika katika taifa la Somalia lililokumbwa na migogoro kimesema kimekamilisha awamu ya kwanza ya kupunguza wanajeshi kwa lengo la kuweka suala la usalama mikononi mwa jeshi la taifa na polisi.
Mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rwanda Paul Rusesabagina, ambaye alifahamika kimataifa kwa juhudi zake za kuwaokoa watu wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994, amesema kuwa Wanyarwanda ni wafungwa ndani ya nchi yao.