Idara ya elimu ya NSW inatarajiwa kutoa uhakika wa ajira kwa takriban walimu 1400, pamoja na wafanyakazi wasaidizi kama sehemu ya mpango wa kuajiri na kuhifadhi kwa shule. Mradi huo unalengo lakuhamisha idadi yawalimu wa muda elfu 10 pamoja na wafanyakazi wasaidizi elfu 6, katika mikataba yakudumu katika hatua ya kwanza, hatimae itafanya nafasi elfu 16 ziwe zakudumu kufukia 2024.
Waziri mkuu Anthony Albanese amethibitisha kuwa Mfalme Charles amepokea mwaliko kutembelea Australia. Hali hiyo imejiri siku chache baada yaku wasilishwa kwa kiapo cha umma kwa sherehe yakutawazwa, ambayo itawaalika raia wote wajamii yamadola kula kiapo cha utiifu kwa Mfalme na warithi wake.
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula Duniani, WFP, Cindy McCain, amesema shirika hilo litaanza tena shughuli za utoaji misaada ya kiutu nchini Sudan, kufuatia mzozo nchini humo kuendelea kupambamoto.
Rais wa Kenya, William Ruto Jumatatu aliongoza sherehe za siku ya wafanyakazi duniani katika bustani ya Uhuru iliyoko katika jiji la Nairobi. Wakati wa maadhimisho hayo, Ruto alichukua nafasi kufafanua mikakati iliyowekwa na serikali yake katika kusaidia baadhi ya sekta zinazokua nchini nchini humo.
Nchini Tanzania wafanyakazi wameahidiwa kurejeshewa mfumo wa nyongeza ya mishahara wa kila mwaka ambayo ilikuwa umesitishwa miaka saba iliyopita na aliyekuwa raisi wa awamu ya tano John Pombe magufuli. Wafanyakazi hao pia wameitaka serikali kusimamia utekelezaji wa sheria za kazi ili kuleta usawa na haki katika maeneo ya kazi na kuepuka na tabia yakuongeza mishahara kama hisani