Taarifa ya Habari 2 Oktoba 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Serikali ya Victoria yaahidi mamia yamamilioni ya dola kuboresha mfumo wa afya ya umma iwapo itashinda uchaguzi wa jimbo ujao.


Serikali ya shirikisho inaomba Optus ieleze Services Australia ni kadi ngapi za Medicare ambazo zime athiriwa na udukuzi wa data za kampuni hiyo. Optus imetoa taarifa kwa wateja wake elfu 10,200 kuwa taarifa zao binafsi zilichapishwa mtandaoni kwa muda. Zaidi ya kadi za Medicare 36,000 zimeripotiwa kuathiriwa katika udukuzi huo ila, kampuni hiyo bado haija jibu maombi ya serikali kwa taarifa maalum.

Daktari raia wa Tanzania anayefanya kazi nchini Uganda aliyeambukizwa Ebola amefariki dunia, mhudumu wa kwanza wa afya aliyefariki kwa ugonjwa huo katika mlipuko wa hivi karibuni nchini humo, waziri wa afya wa Uganda amesema Jumamosi. Mamlaka katika taifa hilo la Afrika Mashariki ilitangaza kuzuka kwa homa kali ya virusi vya Ebola Septemba 20 na kusababisha hofu ya mgogoro mkubwa wa kiafya katika nchi hiyo yenye watu milioni 45.

Burundi hatimae imefungua upande wake wa mpaka kuingia Rwanda siku ya Ijumaa baada ya kukataa kufanya hivyo mapema mwaka huu pale Rwanda ilipoamua kufungua mipaka na jirani yake. Rwanda ilifungua mipaka yake mapema mwaka huu baada ya kufungwa kwa zaidi ya miaka miwili kufuatia mvutano wa kisiasa kati ya nchi hizo jirani. Serikali ya Bujumbura iliendelea kuishtumu Kigali kwa kutowakabidhi kwa vyombo vya sheria vya Burundi watu wanaoshukiwa kushiriki katika njama ya kupindua utawala wa hayati Rais Pierre Nkurunziza tarehe 13 Mei mwaka wa 2015.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service