Msemaji wa upinzani kwa maswala yawa Australia wa kwanza Jacinta Price, amezindua rasmi kampeni ya La ya chama cha Liberals cha WA, kwa Sauti yawa Australia wa Kwanza bungeni. Wakati huo huo chama shiriki cha mseto jimboni humo, WA Nationals Novemba mwaka jana kilitangaza kuwa kita unga mkono kampeni ya Ndio katika kura hiyo ya maoni.
Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS, imeridhia uwezekano wa kuingilia kati kijeshi kurejesha demokrasia nchini Niger, ikiwa juhudi za kidiplomasia zitagonga mwamba. Kamishna wa Mambo ya Siasa, Amani na Usalama Abdel-Fatau Musah ameyasema hayo baada ya kuhitimishwa mkutano wa siku mbili wa wakuu wa majeshi wa mataifa hayo ya Afrika Magharibi uliofanyika mjini Accra Ghana. Katika mkutano huo ambao ulikuwa na lengo la kuharakisha upatikanaji wa vifaa vya kufanikisha uingiliaji wa kijeshi na mikakati yao, hakujwekwa wazi ni lini hasa zoezi hilo linaweza kutekelezwa.
Mwanadiplomasia Wilbroad Slaa amewataka Watanzania kusimama imara katika kutetea na kulinda rasilimali za taifa ambazo zimekuwa zikinufaisha mataifa mengine huku wao wakiendelea kukabiliana na umasikini bila ya kupata manufaa kupitia rasilimali hizo. Dkt Slaa ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuachiwa kwa dhamana na jeshi la polisi lililokuwa likimshikilia kwa takribani siku tano. Dkt Slaa anatuhumiwa na jeshi la polisi kwa uchochezi pamoja na makosa ya uhaini kufuatia kupinga uwekezaji wa bandari kati ya serikali ya Tanzania na Dubai, hivyo amewataka Watanzania kumuunga mkono kuendelea kulinda rasilimali za nchi kwa faida ya kizazi cha sasa na cha baadaye.