Kiongozi wa jimbo la Kusini Australia Peter Malinauskas ametangaza kuwa mto Murray unafungwa kwa shughuli zote ambazo si mhimu. Ameongezea kuwa wakati jimbo hilo linakabiliana na mapito yamaji, ni mhimu kutekeleza sheria mara moja dhidi yakuogelea nakuvua samakai kutoka maeneo ya mpakani hadi Wellington.
Bunge la Victoria limefunguliwa rasmi baada ya ushindi mkubwa wa chama cha Labor mwezi uliopita. Baada ya sherehe ya ukaribisho nchini ndani ya ukumbi wa Queen's Hall, zaidi yawajumbe wapya 40 wali apishwa. Mbunge wa Bendigo West Maree Edwards, amechaguliwa tena kuwa spika wa bunge hilo. Gavana wa jimbo hilo Linda Dessau ametangaza rasmi bunge hilo kuwa wazi katika hotuba yake mapema hii leo Jumanne.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amechaguliwa tena kuwa kiongozi wa chama cha ANC katika mkutano wa chama uliofanyika Johanesburg, Afrika Kusini. Wakati matokeo yanatangazwa na rais wa zamani wa nchi hiyo Khalema Motlanthe watu waliokuwepo kwenye chumba cha mkutano walipiga kelele za kushangilia.
Mfanyabiashara maarufu, mwanasiasa na aliyekuwa gavana wa mkoa wa Katanga, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Moise Katumbi, ametangaza kwamba atagombea urais katika uchaguzi mkuu wa Disemba mwaka ujao 2023. Katika mahojiano na televisheni ya ufaransa, Katumbi amesema kwamba sababu yake kubwa ya kutaka kumuondoa Felix Tshisekedi madarakani katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao ni kutaka kusuluhsiha shida za Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na kulijenga jeshi la nchi hiyo.