Serikali ya Queensland inaiomba serikali ya madola isawazishe msaada unao tolewa kwa waathiriwa wa mafuriko jimboni humo, na msaada unao tolewa kwa waathiriwa wa mafuriko wa New South Wales. Naibu kiongozi wa Queensland Stephen Miles ameomba serikali ya madola, iwekeze mfumo wa msaada wenye thamani ya $771 milioni, na isawazishe malipo ya janga kwa waathiriwa wao wa mafuriko.
Shane Warne ame agwa katika ibada ya mazishi ya faragha mjini Melbourne. Takriban idadi ya watu 80 walihudhuria ibada hiyo, katika klabu ya timu ya AFL ya St Kilda mapema hii leo Jumapili. Jeneza la Bw Warne lilizungushwa ndani ya uwanja huo mara moja baada ya ibada hiyo kama ishara ya heshima, familia yaki ikifuata kwa karibu. Ibada ya pili itafanywa ambako umma uta hudhuria katika uwanja maarufu wa Melbourne Cricket Ground, Melbourne, Victoria tarehe 30 Machi 2022.
Maelfu ya wakazi wa Kilimanjaro nchini Tanzania wamejitokeza kumlaki mwenyekiti wa chama cha upinzani- Chadema, Bwana Freeman Mbowe. Mbowe ameenda kwao Hai, kwa mara ya kwanza tangu atoke gerezani Machi 4, mwaka huu ambako alikaa kwa miezi minane akikabiliwa na tuhuma za ugaidi na uhujumu uchumi.