Waziri Mkuu alisema miaka 50 yama husiano yakidiplomasia na Jamhuri yawatu wa China, kabla ya krismasi mwaka huu itakuwa fanikio mhimu, akidokeza kuwa inaweza kutana na kuondolewa kwa baadhi ya vizuizi vyakibiashara. Maadhimisho hayo yatafanyika rasmi Disemba 21.
Upinzani wa shirikisho ume iomba serikali isitishe muswada wayo wa mahusiano ya viwanda. Sussan Ley ame elezea madhara kwa biashara ndogo kama sababu ambayo serikali haistahili endelea na sheria zake za sehemu ya kazi, akisema biashara ndogo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Australia.
Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Rais wa Rwanda Paul Kagame wamekubaliana juu ya haja ya waasi wa M23 kusitisha mapigano na kujiondoa katika maeneo waliyoteka mashariki mwa Congo, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imesema Ijumaa. Waasi wa M23 wamefanya mashambulizi kadhaa mashariki mwa Congo mwaka huu, ikiwa ni mara yao ya kwanza kurejea kwa kishindo tangu mwaka 2012, na kusababisha mapigano na jeshi ambayo yamesababisha maelfu ya raia kukimbia makazi yao tangu mwezi Machi. Machafuko hayo yalizua mivutano ya kidiplomasia kati ya Congo na nchi jirani ya Rwanda ambapo Congo inaishutumu nchi hiyo kwa kuliunga mkono kundi la M23. Rwanda imekanusha shutuma hizo.
Mataifa ya Afrika yanataka nchi tajiri kugharamia mabadiliko yahali ya hewa.
Mwaka huu pekee bara la Afrika limeshuhudia mafuriko mabaya sana huko Afrika Kusini na miaka kadhaa ya ukame mbaya huko Pembe ya Afrika. Mataifa ya Afrika katika mkutano wa COP27 yamesukuma sana kwa mataifa tajiri kulipa fidia ya hali ya hewa na kuchangia katika mfuko wa “hasara na uharibifu” .