Viongozi wa Uingereza na Umoja wa Ulaya wamesema mlango bado uko wazi kwa makubaliano ya uhusiano wao, wa baada ya Uingereza kujiondoa kutoka Umoja huo kufikiwa.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo Bernard Membe amesisitiza yeye bado ni Mgombea wa nafasi hiyo kupitia chama hicho.
Kampeni za uchaguzi mkuu Marekani zimepamba moto ikiwa zimebaki takriban wiki mbili, kabla ya watu kwenda kupiga kura 3 Novemba, huku Rais Donald Trump na mpinzani wake Joe Biden wakitembelea majimbo yenye ushindani mkali katika siku za mwisho za kampeni.