Taarifa ya Habari 20 Oktoba 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Waziri Mkuu Anthony Albanese ametupilia mbali safari yakuenda Israel, kabla ya ziara ya mazungumzo ya pande mbili Marekani wiki ijayo Oktoba 23, wakati chama cha Labor cha Australia kina sisitiza hakija gawanyika kwa sababu ya mgogoro kati ya Israel na Hamas.


Itakuwa rahisi zaidi kugawa familia katika mfumo wakisehria baada ya mageuzi yakurahisisha mfumo wa sheria ya familia kupitishwa ndani ya bunge la shirikisho. Sheria mpya zilizopitishwa bungeni Alhamis Oktoba 19, pia zitafanya mipangilio ya malezi ya watoto pamoja na mfumo wa mahakama kuwa salama zaidi kwa watoto na, kuona dhana ya "kuchangiwa kwa usawa kwa wajibu ya malezi" ikiondolewa. Mnamo mwaka wa 2017, kamati ya pande zote za siasa bungeni, ilipata kuwa masharti yaliyopo yalikuwa yanachanganya, yalifeli kuweka kipaumbele usalama wa watoto na hayakuwa yakitumiwa ipaswavyo katika hali ambayo ina waweka watoto hatarini.

Moto wa vichaka unaendelea kuwa tisho kwa mali katika eneo la kati ya Queensland, wakaazi wakiwa hawa wezi rejea katika nyumba zao. Queensland Fire and Emergency Services imetoa "onyo la sisalama kurejea" katika eneo la Oyster Creek karibu ya Gladstone Oktaba 20, onyo pia zimetolewa kwa eneo la Deepwater. Wazima moto wame kuwa waki kabiliana na moto ambao umechoma zaidi ya hekta 300 tangu Jumapili Oktoba 15.

Rais Xi Jinping wa China alitetea mradi wa kisera katika ufunguzi wa kongamano la Belt and Road Initiative mjini Beijing akiangazia kile anachosema ni mafanikio ya mpango huo katika muongo mmoja uliopita.

Rais Yoweri Museveni aliapa siku ya Jumatano kwamba vikosi vya Uganda vitawasaka waliohusika na vifo vya muongoza watalii na watalii wawili wa kigeni waliokuwa wakienda fungate katika mbuga ya wanyama.

Kampuni ya Kituruki ya Karpowership imerejesha umeme katika mji mkuu wa Guinea-Bissau baada ya serikali kuanza tena kulipa deni la kampuni hiyo. Waziri wa Uchumi wa Guinea-Bissau, Suleimane Seidi, aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumatano (Oktoba 18) kwamba serikali imeweza kulipa kiasi cha dola milioni 6 kati ya 15 za malimbikizo ambazo inadaiwa. Mnamo mwezi Septemba, kampuni hiyo ilizima usambazaji umeme katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown, kutokana na deni la takriban dola milioni 40.



Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service