Polisi nchini Uganda wanachunguza chanzo cha moto uliokiteketeza chuo kikuu maarufu, kikubwa na cha zamani zaidi nchini humo cha Makerere, kilichopo katikati mwa mji mkuu Kampala.
Mwendesha mashtaka mkuu wa Kenya, Noordin Haji, ameamuru kufanywa kwa uchunguzi wa dola milioni 71 kutokana na kile anachosema ni "ununuzi usiokuwa wa kawaida" uliofanywa na Mamlaka ya Usambazaji wa Vifaa vya Tiba, KEMSA, unaohusishwa na janga la virusi vya corona.
Serikali ya Burundi imeihakikishia Jumuiya ya Afrika mashariki kuwa nchi yao iko salama na inawakaribisha wawekezaji katika sekta mbalimbali kwenda kufanya biashara na nchi hiyo ambayo imekuwa katika machafuko ya kisiasa na kikabila kwa zaidi ya muongo mmoja.