Taarifa ya Habari 20 Septemba 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bajeti ya mwisho wa mwaka wa biashara wa 2021/22, yazua mvutano kati ya serikali na upinzani wa shirikisho kila pande ikidai ipewe sifa kwa ubora wayo.


Seriklai ya shirikisho imetoa onyo kabla yakutoa bajeti ya shirikisho mwezi ujao. Inatarajiwa bajeti hiyo itakuwa bora kwa dola bilioni 50 ila, Mweka hazina Jim Chalmers amesema hali hiyo imesababishwa na maswala ya mpito. Ameonya kuwa watu hawastahili tarajia maajabu yoyote kutoka bajeti ya kwanza ya serikali yake, ambayo itatolewa 25 Oktoba. Wakati huo huo upinzani wa shirikisho unadai sifa kwa nafasi nzuri ya bajeti ya mwisho ya 2021/2022 iliyo fichuliwa hii leo jumanne.

Hayati Malkia Elizabeth II amepumzishwa ndani ya kanisa la mtakatifu George ambalo limo ndani ya kasri ya Windsor. wanachama wa familia yakifalme, walirejea ndani ya kanisa hilo kwa ibada maalum, baada ya siku iliyo jawa mbwembwe nakuwavutia viongozi wakimataifa katika ibada ya mazishi, pamoja nakuvutia umati mkubwa wa watu walio jumuika mitaani kutoa heshima zao za mwisho.

Bunge la Uganda linachunguza sheria iliyopendekezwa ambayo itawezesha upandikizaji wa viungo kufanyika nchini humo kwa mara ya kwanza, na kubadilisha maisha ya maelfu ya watu wanaotarajia operesheni. Mamia ya Waganda, ambao hawawezi mudu gharama hii, wanaishi kwa kutumia dialysis kwa muda mrefu iwezekanavyo. Uganda pia imethibitisha mlipuko mpya wa virusi vya Ebola.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service