Jimboni Qld polisi wame piga mwanaume mmoja risasi naku muuwa mchana wa leo katika eneo la kaskazini Brisbane. Polisi wamesema mwanaume huyo kutoka jamii yawa Australia wa kwanza, walipigwa risasi wakati walikuwa waki jibu wito kwa kesi ya vurugu ya nyumbani katika kitongoji cha Grange. Tukio hilo limejiri siku moja baada ya huduma za dharura kuitwa katika anwani hiyo, kwa sababu ya wasiwasi wa afya ya akili kuhusu mwanaume huyo.
Kiongozi wa chama cha Liberal cha Victoria, John Pesutto, amezomewa na wanao muunga mkono mbunge aliye furushwa kutoka chama hicho Moira Deeming. Katika kongamano la chama hicho mjini Bendigo, kundi dogo lililo kuwa na barakoa ya picha za sura ya Bi Deeming, lili beba mabango yaliyo muita Bw Pesutto mnyanyasaji pamoja naku paza sauti zao wakilalamika neno aibu.
Pande hasimu nchini Sudan, zimekubaliana kusitisha mapigano kwa siku saba kuanzia Jumatatu. Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Marekani, pande hizo kwa mara ya kwanza zimefanya makubaliano na kutia sahihi zao. Taarifa iliyotolewa Jumamosi jioni imesema kwamba makubaliano hayo ya kuweka chini silaha yaliyofanyika mjini Jeddah Saudi Arabia, yanakusudia kuwapa watu wa Sudan nafasi ya kupata misaada ya kiutu.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amewataka Watanzania kuacha kulalamika ugumu wa maisha na badala yake wachukue hatua kwa kuiondoa CCM madarakani.
Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametumia gesi kesi ya kutoa machozi ili kutawanya waandamanaji katika mji mkuu Kinshasa. Maandano hayo yaliitishwa na upinzani uliokuwa ukijimuhisha aliyekuwa waziri mkuu Matata Ponyo, Martin Fayulu, Moise Katumbi na Delly Sesanga wananuia kukemea gharama ya juu ya maisha ya kawaida, ukosefu wa usalama Mashariki mwa DRC na hali ya kutoweka wazi katika maandalizi ya uchaguzi uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu. Gavana wa mkoa wa Kinshasa, Gentini Ngobila pia amelaumu upinzani kutaka kuvuruga usalama wa umma.