Serikali ya Victoria imetupilia mbali mpango wa chama cha upinzani waku wahamisha wagonjwa katika vifaa vya karantini vya Melbourne ambavyo vinakaribia kuwa vitupu.
Madaktari wa viungo wa Australia wametoa onyo la aharaka kwa mamilioni ya waajiriwa, ambao bado wanafanyia kazi nyumbani wakati ripoti mpya imeonesha ongezeko la majeraha ya shingo na mgongo.
Tume ya Umoja wa Mataifa ya ulinzi wa amani nchini DRC imeondoka katika moja ya miji mikubwa mashariki mwa nchi baada ya maandamano mabaya dhidi ya kushindwa kwake kuwalinda raia, maafisa wa Congo na umoja wa mataifa wamesema. Mamia ya wanajeshi na maafisa wa kiraia wameondoka mjini Butembo na majadiliano yamepangwa namna ya kuondoa vifaa vyao , gavana wa jimbo la kivu kaskazini Generali Constan Ndima amewaambia waandishi wa habari.