Mweka hazina wa NSW ametoa bajeti ambayo imezungumziwa kuwa ni ya mara moja katika kizazi, kwa jinsi imewalenga wanawake katika nguvu kazi. Hati hiyo inajumuisha taarifa ya kwanza ya fursa ya wanawake ambayo, kwa sasa ita unda sehemu ya bajeti zote za usoni. Huduma ya malezi ya watoto pamoja na likizo za wazazi zikiwa kipaumbele mhimu, dola bilioni 45 zitatumiwa katika muongo ujao, kwa fursa bora za malezi ya familia na hatua zakuwasaidia wanawake kurejea katika nguvu kazi baada yakujifungua.
Watoto wa Australia wenye chini ya miaka mitano, wanaweza stahiki kupata chanjo za UVIKO-19 katika wiki zijazo. Waziri wa afya, Mark Butler, amesema kuwa mamlaka ya bidhaa za dawa almaarufu TGA, inazingatia ombi kutoka kampuni inayotengeza madawa, Moderna, iruhusu chanjo zake zitolewe kwa watoto wenye miezi sita hadi miaka mitano. Wakati huo huo serikali mpya ime ahidi pia kuunda tume yakifalme, itakayo chunguza majibu ya taifa kwa janga hili ila, Bw Butler hakuweza toa muda wa lini tume hilo lita anza vikao.
Wakuu wa mataifa ya Afrika Mashariki wamekubaliana jana Jumatatu kupeleka jeshi la kikanda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kujaribu kumaliza vita mashariki mwa nchi hiyo. Wakuu wa mataifa ya Afrika Masharikipamoja na kukubaliana kuanzisha jeshi hilo, wametoa pia mwito wa kusimamishwa mapigano mara moja. Wakuu hao walikutana jijini Nairobi kujadili hali ya usalama kwenye eneo hilo.