Data ya malipo ya benki ya Commonwealth imeonesha kuwa wa Australia wana ongeza matumizi yao kwa vitu muhimu kama bima, gharama za matibabu na maduka yamadawa, hali inayo acha sehemu ndogo kwa matumizi ya vitu vya nyumbani na mavazi, vijana wakiwa wame athiriwa zaidi.
Kiongozi wa Magharibi Australia Roger Cook ameondoka jimboni humo aki elekea katika ziara ya biashara China, kwa ajili yaku imarisha biashara na utalii. Kiongozi huyo amesema atazungumza na wawakilishi wa sekta, pamoja na viongozi muhimu wa serikali ya China. China inawajibika kwa 55% ya mauzo yote ya Magharibi Australia.
Waangalizi wa watumiaji wa Australia wame endelea kuhamasisha wateja waendelea kufanya tahadhari kwa utapeli wa mtandaoni, wakati wa Australia wanatarajiwa kutumia zaidi ya bilioni 6 za dola katika mauzo ya Black Friday na Cyber Monday. Ripoti mpya kutoka kampuni ya I-N-G, imefichua kuwa zaidi ya 52% ya watu walio shiriki katika kura ya maoni, wanaweza bonyeza kitufe cha punguzo ya bei katika barua pepe yao bila kuhakikisha ni kiungo halali.
Uamuzi wa Afrika Kusini wa kuipeleka Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa ajili ya uchunguzi wa tuhuma za uhalifu wa kivita uliofanywa na Israel huko Gaza umeibua mijadala mikali ndani na nje ya nchi.
Rais mteule wa Liberia Joseph Boakai aliyemshinda rais George Weah kwenye uchaguzi wa marudio wa Novemba 14 amesema kwamba utawala wake utatathmini upya mikataba ya uchimbaji madini, ili kuhakikisha inanufaisha nchi.
Benki ya Dunia ilisema Jumatatu inatazamia msaada wa dola bilioni 12 kwa Kenya katika kipindi cha mitatu ijayo, utaliboresha taifa hilo la Afrika Mshariki ambalo linakabiliwa na matatizo ya kifedha. Benki hiyo ilisema katika taarifa kwamba jumla ya pesa hizo zitatokana na idhini ya wakurugenzi watendaji wa benki hiyo na vigezo vingine ambavyo vinaweza kushawishi uwezo wake wa kukopesha.