Mamia ya waandamanaji wamejumuika katika sehemu zakati ya mji wa Melbourne kuanzia mida ya saa sita mchana wa leo, wengi wao wakiwa mbele ya bunge ya Victoria, ambako polisi wame jenga mistari mizito ya vizuizi. Inaaminika waandamanaji hao wanatoka katika sekta ya ujenzi hata hivyo, si wazi kama wote ni wanachama wa chama la wajenzi au la.
Milipuko kadhaa imeukumba mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, na kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine kadhaa. Matukio hayo ambayo yametokea jioni ya Jumatatu yameripotiwa na polisi na vyombo vya habari vya taifa hilo. Mashambulizi ya Bujumbura yanafanyika baada ya jengine kutokea katika mji mkubwa wa Gitega, ambako watu wawili waliuwawa na mfululizo wa mizinga iliyolenga uwanja wa ndege wa kimataifa wa taifa hilo usiku wa Jumamosi.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ni miongoni mwa viongozi wachache wanaohudhuria mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York ambao kwa sehemu kubwa unafanyika kwa njia ya mtandao. Karibu viongozi 100 watahudhuria mkutano huo kupitia mtandao baada ya kushauriwa kutokwenda New York katika juhudi za kupambana na janga la COVID-19.