Wazima moto wana wanakabiliana na mioto kadhaa ambayo imeharibu nyumba katika jimbo la Magharibi Australia, na wanakabiliana na siku nyingine ya mazingira magumu.
Upinzani wa shirikisho ume zindua mradi wakutoa uelewa kuhusu unyanyasaji wa nyumbani, kabla ya mwanzo wa msimu wa likizo. Kaimu kiongozi wa upinzani Sussan Ley pamoja na Seneta Kerrynne Liddle, wame waomba wa Australia watumie mitandao yakijamii kuchangia huduma zinazo patikana.
Wakati zoezi la kuhesabu kura likiwa linaendelea katika baadhi ya vituo vyakupigia kura nchini DRC, mjini Goma baadhi ya raia waliojitokeza tena kupiga kura wameshindwa kutekeleza haki yao na kurejea majumbani mwao.
Kuenea kwa mapigano kusini mashariki mwa Sudan kumeyalazimisha mashirika ya misaada ya kibinadamu kusitisha kwa muda operesheni zao kwenye baadhi ya maeneo, wakati UNICEF ikielezea wasi wasi wake kuhusu mamilioni ya watoto walio hatarini kutokana na ghasia zinazosambaa.
Rais wa Benin Patrice Talon siku ya Alhamisi amesema anataka kurejesha uhusiano kati ya nchi yake na nchi jirani ya Niger, ambayo hivi sasa inatawaliwa na viongozi wa kijeshi.