Jumatatu ilikuwa siku rasmi ya watu wengi wenye viza pamoja na watalii wakimataifa kurejea nchini kwa mara ya kwanza katika miaka mbili, hali iliyo zua shangwe na sherehe kote nchini, familia na marafiki walipokutana tena katika takriban kila jimbo. Hali hiyo ilijiri baada ya siku 702 pamoja kufunguliwa kwa baadhi ya vikundi maalum vilivyo chanjwa kutoka ng'ambo.
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi za Umoja wa Ulaya wanakutana Brussels kulijadili suala la mgogoro unaondelea kuhusu Ukraine pamoja, huku shinikizo la kuiwekea vikwazo Urusi likizidi. Ukraine imesisitiza kuwa Umoja wa Ulaya unapaswa kuchukua hatua kuliko kusubiri mpaka Urusi itakapofanya uvamizi.
Wizara ya Afya ya Afrika Kusini imesema Jumatatu kwamba inabadilisha kanuni za chanjo ya COVID-19 kwa ajili ya kusaidia kuongeza kasi ya uchomaji wa chanjo hiyo wakati maambukizi yamepungua na nchi ina chanjo za kutosha. Serikali imepunguza muda wa kuchoma dozi ya kwanza na ya pili ya chanjo ya PFIZER kutoka siku 42 hadi 21 na itaruhusu watu ambao wamepokea dozi mbili za chanjo ya Pfizer kuchoma booster miezi mitatu baada ya dozi ya pili tofauti na ilivyokuwa kusubiri kwa miezi sita. Pia itatoa chaguo kuchanganya na kuoanisha booster kwa watu wazima ambao walipata chanjo moja ya J&J au Pfizer miezi miwili baada ya dozi zao.