Taarifa ya Habari 22 Julai 2023

City - Swahili.jpg

Mweka hazina wa taifa Jim Chalmers ametetea mfumo mpya wa ustawi wakitaifa wa serikali, katika jibu kwa ukosoaji kuwa baadhi ya data inayo tumiwa imepitwa na wakati.


Mfumo huo una tambua mada tano za kufuatilia afya usalama, uendelevu, mshikamano na mafanikio yawa Australia.
Bw Chalmers amesema mfumo huo ni sehemu ya hatua yamakusidi yakuweka watu, maendeleo, haki na fursa katika msingi wa uchumi wa Australia. Ameongezea kuwa mfumo huo uta endelea kuboreshwa, baada ya kupokewa maoni yanayo endelea kutoka jamii, utafiti mpya pamoja na data iliyo boreshwa.

Meli za ujasusi za China zinatarajiwa kutazama kwa karibu mazoezi yakijeshi karibu ya pwani ya Australia, wakati makumi yama elfu yawanajeshi wana jiandaa kwa michezo yakivita. Inatarajiwa meli za jeshi la wanamaji wa China, zita elekea Australia wakati mazoezi hayo yakijeshi yatakapo kuwa yaki endelea. Zaidi ya wanajeshi elfu 30 kutoka nchi 13, watashiriki katika mazoezi ambayo yame pewa jina la Talisman Sabre, ambayo ime anza rasmi hii leo Ijumaa 21 Julai mjini Sydney. Brigadier Damien Hill ni mkurugenzi wa Talisman Sabre, amesema meli hizo za China, zitakuwa huru kuingia katika eneo lakipekee lakiuchumi la Australia.

Jeshi la Polisi la New Zealand lime ahidi kufanya uchunguzi wakina kwa mazingira ya Matu Reid aliye fanya mashambulizi la bundiki mjini Auckland, ambako aliwaua wanaume wawili naku wajeruhi watu wengine 10 katika sehemu ya ujenzi. Jeshi la polisi pamoja na serikali ya NZ, wame ahidi kuchunguza iwapo kulikuwa viashirio kuwa Reid ange endeleza uhalifu wake. Ahadi hiyo imefuata ripoti katika gazeti la NZ Herald, kuwa mshambuliaji huyo alikuwa amefutwa kazi katika sehemu hiyo ya ujenzi siku moja kabla yakufanya shambulizi hilo, na kuwa alipia alikuwa amepewa amri yakubaki nyumbani kwa makosa ya unyanyasaji wa nyumbani.

Umoja wa Mataifa ume zindua muhtasari wa sera mpya yaku kuza amani na usalama. Ajenda hiyo inalenga kuzuia migogoro na umuhimu wa kujenga amani katika wakati wa ongezeko ya mivutano ya kisiasa na ukiukwaji wa haki za binadam. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema muhtasari huo wa sera, unaweka wazi maono yake kwa kuboresha juhudi za pande nyingi kwa amani na usalama kwa misingi ya sheria zakimataifa.

Watu wawili wameuwawa jana na wengine zaidi ya 300 wamekamatwa na polisi wakati wa maandamano ya umma nchini Kenya yanayoongozwa na upinzani.
Makabiliano kati ya polisi na waandamanaji ndiyo chanzo cha vifo hivyo kufuatia maandamano yaliyoitishwa na viongozi wa upinzani ambao wamedai kuwa maandamano hayo yataendelea. Shule za kutwa zimefunguliwa tena baada ya serikali kuhakiki hali ya usalama wa wanafunzi. Kwa upande wao, vinara wa upinzani wa Azimio la Umoja bado hawajaonekana hadharani ila wanasisitiza maandamano yanaendelea. Wito wa kukaa kwenye meza ya mazungumzo bado unatolewa kuwarai kiongozi mkuu wa upinzani, Raila Odinga na Rais William Ruto kufikia mwafaka.  

Katika taarifa za michezo:Timu ya kina dada ya Marekani imeanzisha juhudi zake ya kunyakua taji la tatu mfululizo la Kombe la Dunia la Wanawake kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Vietnam. Katika mechi nyengine mabingwa wa mwaka 2011 Japan wameicharaza Zambia mabao 5-0 katika uwanja wa Waikato nchini NZ. Zambia sasa inakabiliwa na kibarua kigumu kufuzu kwa hatua ya 16 bora, mataifa ya Uhispania na Costa Rica wakiwa wana wasubiri moja baada ya nyingine.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service