Kiongozi mpya wa jimbo la Kusini Australia Peter Malinauskas, ametangaza mageuzi kwa usimamizi wa UVIKO katika jimbo hilo. Ameongezea kuwa baraza lake la mawaziri, lita chukua nafasi ya kamati ya UVIKO-19 ya sasa.
Vikosi vya usalama vya Sudan vilimpiga risasi na kumuua kijana mmoja siku ya Jumatatu wakati wa msako mkali dhidi ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka jana madaktari walisema. Sudan imekumbwa na machafuko makubwa tangu mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba yaliyoongozwa na mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan ambayo yamesababisha maandamano ya mara kwa mara.
Serikali ya Kenya imesema kuwa inatarajia uchumi wake kuimarika kwa asilimia 6% mwaka huu , baada ya kunawiri kwa asilimia asilimia 9.9% katika robo ya tatu ya mwaka wa kifedha wa 2021 pamoja na kuongezeka kwa mapokeo ya fedha kutoka raia wake wanaoishi Ughaibuni.