Huduma ya Jeshi la Polisi la Queensland [[QPS]], limekubali kufanya mageuzi kwa wafanyakazi baada ya ripoti iliyo toa ukosoaji mkali na lawama kwa viongozi kwa tamaduni iliyosambaa ya ubaguzi wa rangi na unyanyasaji wakijinsia katika jeshi hilo la Polisi.
Rais wa Kenya Dr William Ruto amesema kuwa wanajeshi wa jumuiya ya Afrika Mashariki "watahakikisha uwepo wa amani" mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo inakabiliwa na mashambulizi kutoka kundi la waasi wa M23. Katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Kinshasa, Dr Ruto alisema wanajeshi hao wa kikanda "watatekeleza amani kwa wale wenye nia ya kuleta ukosefu wa utulivu." Wanajeshi wa Kenya, waliotumwa kama sehemu ya kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki, waliwasili hivi karibuni katika eneo hilo lenye machafuko.
Serikali ya kijeshi ya Mali Jumatatu ilipiga marufuku shughuli za mashirika yasiyo ya serikali yanayofadhiliwa au kuungwa mkono na Ufaransa, ikiwa ni pamoja na mashirika ya kibinadamu, huku kukiwa na mzozo unaozidi kuwa mbaya kati ya Paris na Bamako.
Waziri Mkuu wa muda wa taifa hilo la Afrika Magharibi Kanali Abdoulaye Maiga alihalalisha hatua hiyo katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii, na kuitaja kuwa ni jibu kwa Ufaransa kusitisha misaada ya maendeleo kwa Mali hivi karibuni.