Utafiti mpya umeonesha kuna idadi ya watu ambao hawana uhakika kwa jinsi yakukabiliana na shinikizo la mikopo ya nyumba. Utafiti wa kampuni yamawakala wa mikopo yakununua nyumba, imeonesha 75% ya walio jibu utafiti huo hawana uhakika kwa jinsi ongezeko la kiwango cha hela taslim cha benki ya hifadhi ya Australia huathiri bajeti ya nyumba zao.
Makabiliano ya kisiasa nchini Kenya sasa yamehamia mahakamani kufuatia matokeo ya uchaguzi wa urais wa tarehe 9 Agosti, 2022. Hii ni baada ya mgombea wa urais wa Muungano wa Azimio La Umoja wa Raila Odinga kupinga ushindi wa Bw William Ruto na hivyo kutangazwa kuwa Rais Mteule na Tume Huru ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC). Tayari Bw Odinga kupitia mawakili wake amewasilisha kesi yake mahakamani kwa mujibu wa sheria ya katiba ya nchi hiyo.
Benki ya dunia Jumatatu imetoa msaada wa dola milioni 300 kwa Msumbiji, kuashiria kurejea kwake nchini humo miaka sita baada ya kusitisha msaada wake wa kifedha kufuatia kashfa ya deni iliyofichwa. Waziri wa fedha wa Msumbiji Max Tonela amesema pesa hizo zitatumiwa kufadhili miradi ya miundombinu ili kusaidia kuimarisha uchumi na kuboresha hali ya maisha katika nchi hiyo.