Uchunguzi wa bunge wazingatia kuongeza idadi ya wabunge ndani ya Nyumba ya Wawakilishi, katika juhudi yakupata uwakilishi wa ziada wa ongezeko la watu nchini Australia. Matokeo ya uchunguzi huo yanaweza sababisha ongezeko la wabunge kutoka 151 hadi 234, kulingana na mageuzi ya kabla.
Jamii zawaislamu nchini Australia zime endelea kuadhimisha mwisho wa Ramadan wikendi hii kupitia sherehe zakitamaduni.
Kiongozi wa Sudan ambaye pia ni mkuu wa jeshi, Abdel Fattah al-Burhan, ameridhia kuhamishwa raia na wawakilishi wa kidiplomasia kutoka katika nchi hiyo iliyomo kwenye mzozo. Mapigano ya Sudan yameingia wiki ya pili.
Polisi nchini Kenya walisema Ijumaa kwamba wamefukua miili ya watu watatu, inayodhaniwa kuwa ya wafuasi wa dhehebu la kidini wanaoaminika walijiua kwa njaa, mashariki mwa nchi hiyo wakati wakati polisi imepanua uchunguzi wake.