Sheria mpya ya usalama mtandaoni ime anza kutumiwa leo, sheria hiyo inasema kwamba intanet haiko juu ya sheria. Waziri wa mawasiliano Paul Fletcher amesema sheria hiyo iliyopitishwa bungeni mwaka jana, ime anza kutumiwa kisheria leo hii Jumapili.
Rwanda na Uganda zimesema kwamba zimefanya mazungumzo ya kirafiki kuhusu kuboresha uhusiano baada ya Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa rais wa Uganda Yoweri Museveni kukutana na rais wa Rwanda Paul Kagame mjini Kigali. Mazungumzo ya jana Jumamosi kati ya Kagame na Kainerugaba, jenerali anayedaiwa kuwa mrithi wa babake yamefanyika baada ya miaka mingi ya mvutano kati ya mataifa hayo mawili jirani.
Serikali ya Uingereza jana iliishtumu Urusi kwa kujaribu kuibadilisha serikali ya Ukraine na utawala unaoipendelea na kusema aliyekuwa mbunge wa Ukraine Yevheniy Murayev anazingatiwa kuwa mgombea anayetarajiwa. Serikali ya Uingereza ilitoa madai hayo kwa kuzingatia tathmini ya kijasusi bila ya kutoa ushahidi wa kuyathibitisha. Haya yanajiri huku kukiwa na vita vya maneno kati ya Urusi na mataifa ya Magharibi kuhusu hatua za Urusi dhidi ya Ukraine.