Taarifa ya Habari 23 Julai 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Mfumo wa sera ya nyumba jimboni Victoria, wapokewa kwa hisia mseto na baadhi ya wadau jimboni humo.


Jeshi la polisi la New South Wales limezindua app ambayo ili undwa kama sehemu ya ahadi yaku hakikisha matokeo bora kwa waathirika wa unyanyasaji wa nyumbani na kifamilia jimboni humo. App hiyo kwa jina la 'Empower You', ime undwa kuandika visa vya unyanyasaji kwa siri kwa ajili yakutoa msaada bora.

Kampeni mpya yakitaifa ime zinduliwa inayo wahamasisha wa australia, wajisajili kuwa wafadhili wa viungo kupiga jeki viwango vyaku okoa maisha kupitia upandikizaji. Idadi ya upandikizaji ilifika juu katika mwaka wa 2018, kabla yaku poromoka sana wakati wa janga la UVIKO.

Takribani raia 20 wa Sudan wameuawa katika mashambulizi ya makombora yaliyorushwa katika maeneo ya makaazi ya mojawapo ya miji muhimu ya Darfur na karibu na hospitali katika jimbo la Kordofan Kaskazini. Chama cha Madaktari kilisema kwamba tangu mapema siku ya Ijumaa, makombora yalirushwa karibu na hopsitali nne katika mji mkuu wa jimbo la Kordofan Kaskazini na kuwaua raia wanne na wengine 45 walijeruhiwa.

Mamia ya watu waliingia mitaani katika mji mkuu wa Gaborone nchini Botswana siku ya Jumamosi kupinga dhidi ya mswaada unaotaka kuhalalisha mahusiano ya jinsia moja.
Maandamano hayo yaliyoungwa mkono na makundi ya kidini, yalifanyika mji mzima kuelezea upinzani wao kwa mswaada ambao una lengo la kutekeleza maamuzi ya mahakama mwaka 2019 yanayounga mkono haki za LGBTQ. Maandamano hayo yanafanyika wakati kuna shinikizo kubwa dhidi ya haki za LGBTQ huko kusini mwa Afrika.

Hisia mseto zimeibuliwa kuhusu iwapo hatua ya Rais William Ruto kutumia nguvu za dola kunyamazisha mahasidi wake wa kisiasa itamfaa au kumgharimu kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Baadhi wa wachanganuzi wa masuala ya kisiasa wanaonya kwamba mbinu hii iliyotumiwa na mtangulizi wake, Uhuru Kenyatta na Hayati Daniel Moi, itayeyusha ushawishi wake katika maeneo mbalimbali nchini. Wakati wa kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu uliopita Dkt Ruto alisema chini ya utawala wake polisi hawataingilia kisiasa katika utendakazi.

Na katika michezo mbichi na mbivu zabainika katika michezo ya NRL na AFL nchini, na baadhi ya timu za shushiwa vichapo vya kihistoria katika kombe la dunia la fifa la mpira wa miguu ya wanawake nchini NZ na Australia


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service