Mamkala nchini Ujerumani zinatarajiwa kurefusha tena muda wa utekelezaji wa vizuizi wakati zikikabiliwa na kuongezeka kwa maambukizi mapya ya visa vya corona.
Darzeni ya maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa jana waliomba kusitishwa mara moja kwa mashambulizi holela na kulenga raia katika jimbo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray, wakitaja pia ripoti za ubakaji na vitendo vingine vya kikatili vya manyanyaso ya ngono.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo amewaongoza viongozi kutoka sehemu mbalimbali duniani na Watanzania kwa ujumla kumuaga aliyekuwa rais wa nchi hiyo, hayati John Pombe Magufuli. Akihutubia wakati wa shughuli ya kitaifa ya kuuaga mwili wa Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Rais Samia amewaondolea hofu wote wenye mashaka kuhusu uongozi wake baada ya kuapishwa kufuatia kifo hicho.