Mweka hazina wa Victoria Tim Pallas ametoa bajeti yake ya tisa na ambayo inazingatiwa kuwa ngumu zaidi, yenye taarifa kamili kuhusu mipango yakulipia ongezeko ya madeni ya jimbo hilo. Bajeti hiyo ina mpango wa malipo yenye thamani ya $31.5 bilioni, inayo jumuisha ongezeko ya kodi kwa biashara kubwa, wamiliki wa nyumba zaku kodi, wamiliki wa nyumba zabiashara, sekta yakamari pmaoja namakato kwa huduma ya umma.
Jaribio lakipekee la Australia la chanjo ya mafua, linaweza ondoa mahitaji ya watu kupata chanjo ya mafua kila mwaka. Watafiti katika hospitali ya Mater mjini Brisbane, wanafanya majaribio ya chanjo mpya ambayo wanatarajia itatoa ulinzi wa muda mrefu dhidi ya kirusi na mabadiliko yake.
Watu wa Sudan wana matumaini kuwa kusitishwa mapigano kwa wiki moja kupisha juhudi za kibinadamu kutamaliza madhila wanayopitia, saa chache kabla ya usitishaji mapigano kuanza kutekelezwa baada ya mfululizo wa matamko ya awali ya makabaliano kukiukwa.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, nchi yenye utajiri wa madini, Felix Tshisekedi, atafanya ziara nchini China kuanzia tarehe 24 hadi 29 mwezi Mei. Katika ziara hiyo rais Tshisekedi anatarajiwa kukutana na rais Xi Jinping ambapo atakagua na kusaini mikataba kadhaa muhimu ya kibiashara.
Watafiti na wadau mbalimbali wa masuala ya elimu wameishauri serikali ya Tanzania kupitia upya rasimu ya mitaala ya elimu iliyotolewa Mei 2023 na kufanya marekebisho katika baadhi ya sera ambazo zinaonekana kutokuwa sawa kabla ya kuanza kwa utekelezaji wake.