Wataalam wa uokoaji wa kasi majini wametumwa katika maeneo ambayo yanatishiwa kwa mafuriko katika kanda ya kaskazini New South Wales, na wakaaji wa mji wa Echuca ambao uko kaskazini Victoria, washauriwa kuondoka nyumbani kwao mara moja.
Kenya na Marekani zinataka mzozo wa Ethiopia kutatuliwa haraka iwezekanavyo, nchini Uganda, watu 65 wameambukizwa Ebola wakati, watu 27 wamefariki. Na Umoja wa Mataifa umeonya kwamba hali ya ukame ni mbaya sana Somalia.