Taarifa ya Habari 24 Aprili 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Waziri Mkuu amerudia ahadi ya chama cha mseto kuto ongeza au kuwasilisha kodi yoyote mpya, chama chake kikishinda uchaguzi mkuu.


Chama cha Labor kime ahidi kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya 500 wa ziada kutoka jamii yawa Australia wa kwanza, pamoja nakuwekeza katika tiba zakuokoa maisha za ugonjwa wa figo na ugonjwa wa moyo.

Wafaransa wana piga kura leo Jumapili kwa duru ya mwisho ya upigaji kura katika uchaguzi wa rais, huku Marine Le Pen wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally akiwa pointi chache tu nyuma ya Emmanuel Macron. Ushindi wa Le Pen utakuwa na athari kubwa kwa usalama wa Ulaya kufuatia uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine.

Kenya itafanya mazishi ya kitaifa wiki ijayo ya rais wa zamani Mwai Kibaki, ambaye aliliongoza taifa hilo la Afrika Mashariki kwa zaidi ya muongo mmoja, Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiangi alisema Jumamosi. Kibaki, ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 90, alihudumu kama rais wa tatu wa nchi hiyo kuanzia Desemba 2002 hadi Aprili 2013, akichukua hatamu kutoka kwa utawala wa kimabavu wa Daniel arap Moi.

 


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service