Kuna uwezekano jimbo la New South Wales, linaweza toa chanjo za mafua bure msimu huu. Waziri wa Afya Brad Hazzard amesema hatua hiyo inazingatiwa na maafisa wa afya, kwa sababu msimu huo umegonga jimbo hilo vibaya kuliko miaka ya nyuma. Chanjo za mafua kwa sasa ni bure jimboni NSW kwa watoto ambao wana chini ya miaka mitano, watu wenye magonjwa sugu, wanawake wajawazito, wa Aboriginal na Torres Strait Islanders na watu wenye zaidi ya miaka 65. Kauli hiyo imefuata tangazo kama hilo kutoka Queensland, ambako serikali ya jimbo hilo imewahamasisha watu wachukue faida ya chanjo bure, idadi ya kesi za mafua zinapo endelea kuongezeka sana.
Serikali ya Tasmania inatengeza rasimu mpya ya sheria ya ulinzi wa watoto, ambayo itaruhusu kufungua makosa ya jinai kwa mtu yeyote katika sehemu ya mamlaka, anaye weka mtoto katika hatari ya unyanyasaji. Kiongozi wa jimbo hilo Jeremy Rockliff amesema, muswada huo utafanyiwa rasimu na unatarajiwa kupitishwa katika bunge la jimbo mwaka huu. Hali ambayo ita unda kosa jipya la jinai kwa kufeli kumlinda mtoto au kijana.
Umoja wa Mataifa umeshutumu mashambulizi dhidi ya kambi zake za kijeshi yaliyofanywa na kundi la waasi wa M23 na kulitaka kundi hilo kuacha mapigano mara moja. Taarifa iliyoandikwa na umoja huo kwenye ukurasa wa twitter imesifu juhudi zilizochukuliwa na wanajeshi wake kujibu mashambulizi ya waasi hao. Waasi wa M23 wanawashutumu wanajeshi wa Umoja wa mMataifa kwa kushirikiana na wanajeshi wa serikali pamoja na makundi ya waasi, kushambulia ngome zake.