Serikali ya shirikisho ina jiandaa kuwekeza zaidi katika nishati mbadala, chini ya mpango waupanuzi wake wa uwezo unao fadhiliwa na walipa kodi. Tangazo hilo limejiri katika jibu kwa ongezeko la wasiwasi kwa joto katika majira ya joto, ambayo inaweza ongeza mahitaji ya umeme na kuongeza uwezekano wa ukosefu mkubwa wa umeme. Ni sehemu ya mpango wa serikali, waku fikia utoaji wa 80% wa nishati mbadala kufikia 2030.
Mioto ya vichaka ambayo haija dhibitiwa, ime teketeza angalau nyumba 10 katika mji wa Perth, ila ime pungua kwa sasa. Mamlaka walionya usiku wakuamkia kuwa, upepo mkali na nyuzi joto za juu inamaa inaweza kuwa siku kadhaa kabla wazima moto waweze dhibiti mioto hiyo, iliyo sambaa katika mali ambazo ziko katika mali zenye ziko vijijini nakutishia nyumba zingine. Ilikuwa kuchelewa Alhamisi kwa watu wengi kuondoka katika vitongoji vinane katika miji ya Wanneroo na Swan, ambayo iko katika eneo la Kaskazini mashariki ya Perth.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa siku ya Jumatano alipokea vyema makubaliano ya kusitisha mapigano ya siku nne huko Gaza na kusema anatumai makubaliano kati ya Israel na Hamas yataimarisha juhudi za kufikia mwisho wa mzozo wao. Ramaphosa amekuwa mmoja wa sauti maarufu katika bara la Afrika kuhusu vita vya kikatili kati ya Israel na Hamas ambavyo vimeendelea kwa takriban wiki saba.
Rais wa Kenya William Ruto amesema Alhamisi serikali ya Kenya inaelekea kubinafsisha makampuni 35 ya umma na ilikuwa inayaangazia makampuni mengine zaidi 100 baada ya kupitisha sheria mwezi uliopita kuondoa urasimu.