Wanafunzi kuanzia darasa la pili hadi 11 jimboni New South Wales, watarejea darasani kesho Jumatatu 25 Oktoba kwa mara ya kwanza baada ya miezi mingi. Hata hivyo shule tisa zimefungwa kwa muda kwa ajili yakufanyiwa usafi, baada ya kesi za Uviko kutambuliwa tangu shule zilipofunguliwa kwa wanafunzi wiki iliyopita.
Wanao ishi Melbourne na katika kanda ya Victoria wataweza kutana tena wiki hii, wakati jimbo hilo lina regeza vizuizi zaidi. Usafiri jimboni humo utaruhusiwa tena kuanzia tena Ijumaa 29 Okt, saa 12 jioni, wakati 80% ya chanjo inatarajiwa kutolewa. Barakoa hazita hitajika kuvaliwa nje na ndani ya kumbi za burudani, katika sehemu ya mazoezi na ndani yamaduka kwa wateja ambao wame pata chanjo kamili.
Polisi nchini Uganda imesema mtu mmoja ameuwawa na wengine 7 kujeruhiwa katika mlipuko mkubwa katika mji mkuu Kampala. Tukio hilo ambalo Rais Yoweri Museveni amelitaja kuwa la kigaidi, linaripotiwa kutokea majira ya saa tatu usiku wa kuamkia leo katika mgahawa maarufu ulioko mtaa wa Kawempe kaskazini mwa Kampala.