Taarifa ya Habari 24 Oktoba 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Wa Australia ambao wamekwama mjini Gaza, wamesema wameshauriwa mara kwa mara waende katika kivukio cha mpaka wa Rafah na Misri, hata hivyo walipofika huko walipata mpaka huo umefungwa.


Jeshi la polisi la New South imesema chunguza chanoz cha mioto kadhaa katika neo la pwani ya kati kaskazini, ambayo wana amini inamashaka, wakati mioto inaendelea kuwaka jimboni humo. Hali hiyo imejiri baada ya mioto kukabiliwa katika maeneo ya Nymboida, karibu ya Grafton, na karibu ya mji wa Penrith ambao uko katika eneo la maghabi Sydney ambako mioto hiyo ili dhibitiwa Jumatatu Oktoba 23.

Wakaazi wa maeneo ya vijiji vya Kusini Queensland, wame hamasishwa waondoke katika maeneo hayo kwa sababu maisha yao yanaweza kuwa yako hatarini kupitia moto wa vichaka unao sambaa kwa kasi. Shirika la Queensland Fire and Emergency Services, hii leo lime toa onyo lingine kwa wakaazi waondoke katika maeneo ya Tara na Kogan, wakati kituo cha kupokea watu kimeandaliwa katika eneo la Western Downs Regional Council customer contact centre.

Wanasheria nchini Tanzania wameitaka serikali kuweka wazi mikataba mitatu ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na DP World ili kuhakikisha maoni ya wananchi yamesikilizwa na kufanyiwa kazi. Wakati uwekezaji huo unatarajiwa kuongeza ufanisi katika uendeshaji na utoaji huduma pamoja na kuongeza ajira kwa Watanzania.

Nchi wanachama wa umoja wa ulaya jumatatu zimepitisha muundo wa kuwawekea vikwazo maafisa wa utawala wa kijeshi walionyakua madaraka Niger mwezi julai. Utaratibu huo mpya utairuhusu EU kuweka vikwazo kwa watu binafsi na taasisi zinazohusika na vitendo vinavyotishia amani , utulivu na usalama wa Niger, kudhoofisha utaratibu wa kikatiba au kujumuisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu au sheria za kimataifa za kibinadamu , baraza la EU limesema.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 24 Oktoba 2023 | SBS Swahili