Serikali ya shirikisho ita anzisha sajili mpya kwa ulaghai wa ujumbe wa simu za rununu, wakati idadi kubwa yawa Australia wanaendelea kuwa waathiriwa wa ulaghai mtandaoni.
47% yawa Australia wameripoti kuwa wamepokea jumbe fupi za sami kutoka kwa walaghai, katika mwaka uliopita wakati wa Australia walipoteza zaidi ya bilioni 3 za dola kupitia ulaghai katika mwaka wa 2022. Dola milioni 10 zitawekezwa, kuzindua sajili hiyo mpya katika bajeti ya shirikisho mwezi ujao.
Majenerali wanaopingana nchini Sudan wamekubali kusitisha mapigano kwa siku tatu kuanzia usiku wa kuamkia hii leo Jumanne licha ya makubaliano ya hapo awali kuvunjika ndani ya muda mfupi. Wakati ambapo serikali za kigeni zikiendelea na zoezi la kuwahamisha mamia ya wanadiplomasia wao pamoja na raia wao kuwapeleka mahala salama, Wasudan wanahangaika kutafuta njia za kuepuka machafuko hayo, wakihofia kwamba pande mbili za jeshi zinazopingana nchini humo zitazidisha vita vyao vya kuwania madaraka mara baada ya nchi za kigeni zitakapomilisha shughuli za kuwaondoa raia wao.
Idadi ya waliofariki katika tukio lililohusisha dhehebu la Kenya lililoamuru waumini wake kukaa na njaa hadi kufa iliongezeka na kufikia 73 Jumatatu, vyanzo vya polisi vimeiambia AFP. Wanaofanya uchunguzi walifukua maiti zaidi kutoka kwenye makaburi ya watu wengi katika msitu karibu na pwani. Uchunguzi ulianzishwa dhidi ya kanisa la Good News International Church na kiongozi wake Paul Mackenzie Nthenge ambaye alitajwa katika hati za mahakama, ambaye alihubiri kuwa kifo cha njaa kitawafikisha waumini kwa Mungu.