Taarifa ya Habari 25 Julai 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Waziri Mkuu Anthony Albanese, amesema Australia inahitaji jiandaa kwa msimu wa moto wa vichaka ujao, wakati mioto ya vichaka inaendelea kuchoma maeneo ya Kaskazini ya dunia.


Chama cha ujenzi, misitu, madini na nishati kinaomba pawe kodi ya faida ya super, kuwekeza kwa ujenzi hatua itakayo tatua janga la utoaji wa nyumba nchini Australia.

Idadi kubwa yawa Australia wamejisajili kupiga kura, katika kura ya maoni ijayo kwa sauti yawa Australia wa kwanza bungeni. Tume ya uchaguzi ya Australia imekadiria kiwango chakitaifa cha usajili kimefika 97.5% kutoka 97.1% kwa takwimu za mwisho wa 2022.Idadi kubwa yawa Australia wamejisajili kupiga kura, katika kura ya maoni ijayo kwa sauti yawa Australia wa kwanza bungeni. Hii inamaana kura ya maoni ya 2023 itakuwa na msingi bora kwa ushiriki wakidemokrasia, kuliko tukio lingine la uchaguzi wa shirikisho katika historia ya Australia.

Vyama vya kisiasa nchini Tanzania sasa vimeanza kutumia majukwaa ya wazi na mikutano ya hadhara kuwashawishi wananchi juu ya kile kilichomo kwenye mkataba wa bandari kati ya nchi hiyo na kampuni ya kigeni ya DP World.

Jenerali mmoja wa Sudan alikataa akitoa lugha ya vitisho pendekezo lililoongozwa na Kenya kwamba walinda amani wa Afrika Mashariki wasaidie kumaliza vita vya zaidi ya siku 100 nchini Sudan katika video iliyotolewa Jumatatu na kukosolewa vikali na mamlaka ya Kenya.

Siku chache baada ya polisi kuvamia nyumba ya mwanawe Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, Jomo, Mkuu huyo wa zamani wa Nchi kwa mara nyingine amezungumza kuhusu kisa hicho akidai kuwa kulikuwa na mpango wa kumwekea bunduki na dawa za kulevya wakati wa operesheni ya Ijumaa usiku.



Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service