Serikali ya New South Wales imesema itaharakisha jaribio la kuwaruhusu madereva kupunguza alama moja ya adhabu, kama wameonesha rekodi nzuri yakuendesha gari.
Utafiti mpya unatabiri kuwa idadi yawatu wazima wanao ishi na ugonjwa wa kisukari kote duniani ita ongezeka mara mbili kufikia 2050. Utafiti huo unalaumu kuongezeka kwa kasi kwa viwango vya fetma, na kuongezeka kwa uhaba wa usawa katika afya kwa watu wazima bilioni 1.3 ambao watakuwa na kisukari ndani ya miongo ijayo.
Mamluki wa kampuni binafsi ya kijeshi ya Wagner wameanza leo kurejea kwenye kambi zao baada ya kiongozi wao Yevgeny Prigozhin kukubali kwenda uhamishoni nchini Belarus.
Umoja wa Mataifa, Jumamosi umetoa mwito wa kuchukuliwa hatua za haraka kukomesha mauaji ya kiholela ya watu wanaokimbia El Geneina, mji mkuu wa jimbo la Darfur Magharibi, na wanamgambo wa kiarabu wakisaidiwa na wanajeshi wa jeshi la taifa.