Vizuizi vya COVID-19 vime anza kutekelezwa katika maeneo ya jiji la Melbourne, kesi zingine tano zikiwa zimeungwa na mlipuko katika eneo la kaskazini la mji huo.
Idadi hiyo imefikisha idadi ya watu wenye virusi hivyo kufika watu tisa. Baadhi ya vizuizi hivyo vinajumuisha amri yakuvaa barakoa watu wakiwa ndani yamajengo, pamoja na vikomo kwa idadi yamikusanyiko ya umma. Kesi nne zilitangazwa mchama wa leo jumanne, zimeungwa na kesi iliyo fichuliwa asubuhi ya leo inayo husu mwanaume mwenye umri wa miaka 60, ambaye mamlaka wa afya wameunga kwa mlipuko wa familia moja katika eneo la Whittlesea.
Tukisalia jimboni Victoria, shirika la Kidsafe Victoria limezindua kampeni mpya ya uelewa baada ya idadi yawatoto 32, inayo husu mtoto mmoja kila siku 11 kufariki kupitia majeraha yanayo weza zuiliwa katika jimbo hilo mwaka jana. Takwimu kutoka kitengo cha uchunguzi cha majera cha Victoria, zimeonesha kuwa idadi ya watoto elfu 13,843 wenye umri kati ya miaka 0-14 wali lazwa katika hospitali za Victoria, kwa sababu yamajeraha yasiyo yakukusudiwa katika mwaka wa 2020.