Mafuriko yanaendelea kukabili sehemu za Victoria, utata ukisambaa katika mji wa Echuca kuhusu jinsi yakuondoa maji hayo yamafuriko. Mji huo wa mpaka wa mto Murray umetengwa kwa ukuta wa vizuizi ambavyo, vimewekwa katika mitaa kulinda maeneo ya kati ya mji huo. Ila wakaaji katika nyumba zilizo upande wenye vizuizi, wameshangazwa kuona maji yakielekezwa katika maeneo yao ambayo yame athiriwa tayari kwa mafuriko.
Kampuni ya bima ya afya ya Medibank, imefunguka kuwa udukuzi wa data wa wiki jana, ulikuwa mkubwa zaidi kuliko ilivyo dhaniwa kwa mara ya kwanza, idadi ya waathiriwa ikitarajiwa kuongezeka. Medibank imesema inawasiliana na wateja wake wa sasa nawazamani, ambao huenda taarifa zao za faragha zili ibwa baada yakupokea hati zaidi kutoka kwa wadukuzi.
Mamlaka Huru ya Kutathimini Utendajikazi wa Polisi nchini Kenya, IPOA imeanzisha uchunguzi wa haraka kufuatia kitendo cha maafisa wa polisi katika kaunti ya Kajiado kumpiga risasi na kumuua mwanahabari maarufu wa Pakistani Arshad Sharif Jumapili usiku. Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif amezungumza na Rais wa taifa hilo William Ruto kuhusu kifo cha mwanahabari huyo ambaye polisi nchini Kenya wanasema ni kisa kilichotokea kimakosa.