Wa Australia ambao wana matatizo ya pumu, wame onywa wajiandae kwa kilele cha msimu wa dhoruba ya pumu inayo karibia. Wataalam wamesema kuwa tukio la hali ya hewa la, La Nina huwaweka watu wenye mzio hatarini wakati huu wa mwaka. Kilele cha msimu wa dhoruba ya pumu huanza, mwanzo wa Oktoba na hudumu hadi mwisho wa Disemba. Hiyo ni kwa mujibu wa baraza lakitaifa la pumu, ambayo imesema Australia inamoja ya viwango vya juu zaidi duniani vya pumu, ambayo huathiri mtu mmoja kati ya watu 10.
Benki kuu ya Tanzania itapunguza mzunguko wa fedha katika uchumi mwezi Septemba na Oktoba ili kupunguza kasi ya mfumuko wa bei katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, taarifa ya kamati ya sera ya fedha ya benki hiyo (MPC) iliyochapishwa Jumamosi ilieleza. Uamuzi huo wa sera unalenga kupunguza shinikizo la mfumuko wa bei, huku ikilinda shughuli za kiuchumi.
Wagonjwa wengine watatu wa Ebola wamefariki nchini Uganda, wizara ya afya imesema Ijumaa, na kufikisha idadi ya vifo kuwa vinne, siku kadhaa baada ya maafisa kuthibitisha mlipuko wa aina mpya ya ugonjwa huo mbaya ambao chanjo yake haijaidhinishwa bado.