Taarifa ya Habari 26 Aprili 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Maswala ya gharama ya maisha, yanaendelea kujitokeza katika kampeni ya uchaguzi mkuu.


Wanafunzi wa shule za upili wa Kusini Australia, wata takiwa kuendelea kuvaa barakoa katika shule kupunguza maambukizi ya UVIKO-19. Baraza la usimamizi wa dharura wa jimbo hilo limesema, sheria ya barakoa itaendelea kutumiwa kwa wiki nne za kwanza za mhula kuanzia wiki ijayo. Wanafunzi wa shule za msingi hawata lazimishwa kufuata mwongozo huo ila, walimu wote katika shule za msingi na sekondari wata takiwa kuvaa barakoa.

Chama cha wafanyakazi wa huduma ya afya kimesema ombi lake la malipo ya juu kwa wafanyakazi wa huduma ya wazee, ni kesi mhimu zaidi ambayo ime wahi simamia. Chama hicho, kime wasilisha kesi yake ya malipo ya juu kwa tume ya usawa wa kazi hii leo Jumanne 26 Aprili 2022, kikisema wanachama wake wanastahili pewa nyongeza ya mshahara ya 25%.

Watu 16 wakiwemo wanajeshi tisa walifikishwa mahakamani siku ya Jumatatu nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wakituhumiwa kuuza silaha kwa kundi la wanamgambo huko kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo. Silaha za jeshi zinashukiwa kuangukia kwenye mikono ya kundi lenye sifa mbaya la CODECO linalolaumiwa kwa mauaji ya kikabila katika jimbo la kaskazini-mashariki la Ituri. Silaha hizo zinadaiwa zilitumika katika mashambulizi kwenye vijiji na kambi za watu wasiokuwa na makazi. Wanajeshi tisa walioshtakiwa ni pamoja na lutein kanali na mameja watatu.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service