Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani limewasilisha hati ya mashtaka mbele ya Baraza la Seneti dhidi ya rais wa zamani Donald Trump na kufungua njia ya kuanza kwa shauri la pili la kihistoria.
Mahakama moja Uganda imeamuru vikosi vya usalama kuacha kuzingira nyumba ya kiongozi wa upinzani Robert Kyagulani anayejulikana pia kwa jina lake la usanii Bobi Wine. Wine alikuwa anazuiliwa nyumbani kwake tangu uchaguzi wa rais katikati ya mwezi na kumesababisha shinikizo la kimataifa aachiliwe, wakili wake alisema Jumatatu.
Gavana wa Kivu Kaskazini anawasihi raia kushirikiana na jeshi kusitisha uasi. Amesema juhudi za jeshi pekee hazitoshi, ikiwa wananchi hawatatoa mchango kamili katika kufanikisha suala hilo.