Queensland yajiandaa kuanza kuwapokea tena wanafunzi wakimataifa punde baada yakukamilika ujenzi wa makazi ya karantini mjini Toowoomba, na Kusini Australia kufungua mipaka yake yote kwa watu ambao wamepata chanjo kamili za Uviko-19.
Umati wa watu umefanya maandamano hadi jana usiku nchini Sudan kupinga mapinduzi ya kijeshi, huku vurugu zikiugubika mji mkuu Khartoum baada ya wanajeshi kuwafyatulia risasi waandamanaji na kudaiwa kuwauwa watu watatu.
Kampuni ya dawa ya Aspen ya Afrika kusini yajipanga kutengeneza chanjo zaidi za COVID-19. Aspen inakusudia kuongeza uwezo wake wa utengenezaji wa chanjo ya COVID-19 hadi dozi bilioni 1.3 kwa mwaka ifikapo Februari mwaka 2024 kutoka kwenye pato la sasa la dozi karibu milioni 250 kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Stephen Saad